Fasihi kwa kiswahili: Kazi za sanaa za fasihi ya Kinyarwanda au ya Kirundi au ya Kiingereza zikiandikwa kwa Kiswahili haziwezi kuitwa kazi za fasihi ya Kiswahili. Hili linatokana na kuwa ili kazi ya fasihi iingizwe katika fasihi ya Kiswahili ni lazima:
a. izungumzie utamaduni wa Waswahili;
b. na itungwe katika Kiswahili.
Bali fasihi kwa waswahili ni zile kazi sanaa ambazo zinashughulikia mambo yanayohusu waswahili wenyewe kama utamaduni wao na mila na desturi zao pia huandikwa katika lugha ya kiswahili.